Tuzo ya kwanza ya AU bila ya magurudumu
Katuni iliyopewa jina " Je tumeshafika?" imechorwa na mchoraji wa
Afrika Kusini John Swanepoel na Jonh Curtis. Katika nchi yao
wanajulikana kama "Dr. Jack & Curtis." Wachoraji hao wameshika
nafasi ya kwanza katika shindano la tatu kwa mwaka huu la uchoraji
katuni la Ujerumani " Third World Journalist Net" Kwa mwaka huu, mada
kuu ya shindano hilo la kimataifa ilikuwa "Miaka 50 ya umoja wa Afrika"
Namba tatu: Mvutano
Samuel Mwamkinga kutoka Tanzania amekuwa mshindi wa tatu. Mchoro wake umeweka wazi changamoto za Umoja wa Afrika.
Tundu katika sehemu ya pili
"Umoja ni muhimu kwa kudumisha Afrika." Hivyo ndivyo ambavyo Victor
Ndula kutoka Kenya alivyoupa mchoro wake jina. Alipata nafasi ya katika
shindano la kuchora katuni.
Mbwa anaebwaka hawezi kuuma
Baadhi ya washiriki wa mashindano hayo wanaonesha nafasi ya Afrika
katika siasa za kimataifa. Miongoni mwa hao ni Ssentongo Jimmy Spire
kutoka Uganda aliechora katuni iliyoitwa "Muungano kwa ajili ya usemi"
Mzigo mzito
Mchoro wa Junior Heritier Bilaka kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya
Congo vilevile unaelezea ushawishi mataifa yenye nguvu duniani kwa
wanasiasa wa Afrika.
Kwa mwendo wa Konokono
Mtazamo wa Tayo Fatunia kwa maadhimisho ya miaka 50 ya Umoja wa Afrika sio mzuri.
Upya wenye mizizi ya zamani
Hivi ndivyo ambavyo Haswel Kunyunye kutoka malawi alivyoweza
kuuelezea iliyokuwa Umoja wa nchi huru za Afrika (OAU) mpaka sasa Umoja
wa Afrika (AU)
Africa ni kirago chenye viraka
Mchora katuni kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Michael Maloji M. Anaonesha mtazamo wake kuhusu Afrika
Msingi wa Umoja
"Miguu ya Afrika" ni jina la kielelelezo kilichowasilishwa na Siphiwo
Sobopha kutoka Afrika Kusini. Michoro zaidi ya katuni inapatikana
katika www.cartoon-competition.org.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !