Headlines News :
Home » » SHEIKH PONDA ANGURUMA DAR ES SALAAM

SHEIKH PONDA ANGURUMA DAR ES SALAAM

Written By kunta kinte on Monday, June 3, 2013 | 3:41 PM

 
Picture
Imamu wa Msikiti wa Mtambani Imam Suleiman akimkaribisha Sheikh Ponda kuhutubia Waislam kwenye Kongamano hilo.
WAISILAM leo wametoa msimamo juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea nchini wakati wa kongamano lililoandaliwa na Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu Tanzania na kufanyika jijini Dar es Salaam.

Kwenye kongamano hilo ambalo masheikh mbalimbali wakiwemo Sheikh Ponda Issa Ponda, Ally Basaleh, Mussa Kundecha na Kondo Juma Bungo waliwasilisha mada mbalimbali pamoja na kutangaza maazimio ya kongamano hilo.

Moja ya mambo yaliyozungumzwa ni mapendekezo waliyowasilisha kwenye Tume ya katiba mpya ambapo 
walisema iwapo mapendekezo waliyowasilishwa hayakuzingatiwa na kutupwa yote basi waisilamu watatangaza kusimamisha mchakato huo nchi nzima na kufanya maandamano usiku na mchana.

Hoja hiyo ilikuja baada ya kunukuliwa kauli ya Waziri wa nchi Sera na Uratibu wa bunge Wiliam Lukuvi, wakati akijibu swali la Mbunge Asumta Mshama aliyetaka kujua kwamba lini serikali itaacha kupanga siku ya kupiga kura kuwa Jumapili wakati wanajua siku hiyo ni siku ya ibada ya Wakristo haioni inawadhulumu haki yao yakufanya ibada? Lukuvi kwenye jibu lake alisema suala hilo limekuwa likilalamikiwa na watu wengi tu lakini serikali kwenye hilo haina utaratibu maalum wa siku ya kupiga kura ila kwakuwa kuna mchakato wa katiba mpya hilo litazingatiwa.

“Hii ni kinyume kabisa na utaratibu wa tume ya katiba. Waziri huyu anataka tuamini kwamba anayafahamu yatakayokuwemo kwenye Katiba Mpya kabla hata wananchi hawajapelekewa na hata haijaandikwa? Hivyo iweje Waisilamu wanaodai siku ya Ijumaa iwe ya mapumziko kwa miaka nenda rudi hawapewi, Wakristo wanakosa siku moja tu ndani ya miaka mitano majibu yanapatikana kirahisi?” Alihoji Sheikh Ponda.

“Waisilamu wamekuwa wakiomba ruhusa kwa mabosi wao siku ya Ijumaa kwenda kufanya ibada na mara nyingine wananyimwa ruhusa hiyo, lakini hakuna vurugu yoyote waliofanya. Wanadai haki hiyo kwa miaka yote hii hawapewi, lakini wengine wanadai kirahisi na kujibiwa kwa uhakika.” Alifafanua Ponda.

Sheikh Ponda ameiomba serikali kuunda tume kwa lengo la  kushughulikia madai ya Waisilam nchini ili kuepusha migogoro ya mara kwa mara dhidi yao pia, akawataka Waislamu wavumilie na wasubiri rasimu itakapotangazwa kwenye magazeti ya serikali. Akaonya kuwa kama mapendekezo waliyowasilishwa yatapuuzwa, basi hakutakuwepo na Katiba Mpya bali maandamano usiku na mchana nchi nzima.

“Tunaiomba serikali iunde tume kushughulikia madai yetu sisi Waislamu tofauti na hivyo tutadai haki zetu kupitia maandamano makubwa ambayo yatafanyika mchana na usiku hadi kieleweke,” alisema Ponda.

Akizungumzia Katiba mpya, Ponda alisisitiza kuwa maoni ya Waislamu yasipoingizwa katika katiba patachimbika bila kufafanua kitakachotokea.

Sheikh Ally Basaleh alisihi Serikali kuwasikiliza Waisilamu hoja zao na wasiwapuuze.
‘Hatugombani na Wakristo’

Naye Sheikh Nassoro Majid amesema Jumuiya na na Taasisi za Kiislamu Tanzania hazina ugomvi na Wakristo bali serikali iliyoshindwa kusimamia haki za Waislamu.

Alisema Waislam wanasikitishwa na kauli za kupandikiza chuki zinazowahusisha na ugomvi wa kidini baina yao na Wakristo.

“Uislamu ni dini ya amani, hatuna ugomvi na wenzetu Wakristo. Mgomvi wetu ni serikali inayoshindwa kutupa na kusimamia haki ya kielimu na nyinginezo,” alisema.

Sheikh Majid alisema wameafanya kongamano hilo kwa lengo la kujadili jinsi ya kuimarisha umoja, kutathmini matukio mazito na kuangalia upepo wa uhusiano nchini na maazimio ya msimamo na muelekeo wa Waislam katika kudai haki zao.

Alibainisha kuwa Wakristo hawana sababu ya kuhofia tofauti za kiimani na wafahamu Waislam hawawezi kugombana nao.

Kwa upande wake, Sheikh Kondo Bungo, akizungumza katika kongamano hilo aliwataka Waislamu na Wakristo kuungana kutafuta adui anayewachonganisha.

Aliitaka serikali kupitia Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Emmanuel Nchimbi kuwapa majibu ya kile kilichobainika na  Shirika la Upelelezi la Marekani FBI katika mauaji ya Padre Evaristus Mushi yaliyofanyika huko Zanzibar.

Source: http://www.wavuti.com/4/post/2013/06/sheikh-ponda-ahutubia-kongamano-la-waislam-dar-es-salaam-na-kuhoji.html#ixzz2VCB2Akz1
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Popular Posts

Comments

blogs zinazotamba

Translate

Popular Post

Flag Counter
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. NDOANO YA HABARI - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template