Mechi ya Kirafiki Maalum iliyoshirikisha Manguli wa Klabu za Manchester United na Real Madrid ili kusaidia Mfuko wa Hisani wa Klabu ya Manchester United uitwao RED HEART UNITED na Real waliibuka kidedea kwa kushinda Bao 2-1.
Kabla ya Mechi hiyo kuanza, kulikuwa na utangulizi wa Shoo Laivu ya Muziki iliyofanywa na Mastaa JLS na Amelia Lily.Real ndio walitangulia kupata Bao lililofungwa na Morientes katika Dakika ya 40 kwa shuti la nje ya Boksi lililomshinda Kipa Edwin Van Der Sar.
Man United walisawazisha katika Dakika ya 67 baada ya Andy Cole kumtengenezea Ruud Van Nistelrooy aliefunga kwa Shuti kali.
Van Nistelrooy alianza Mechi hii kwa kuichezea Real Kipindi cha Kwanza na Kipindi cha Pili kuvaa Jezi ya Man United.
Bao la ushindi kwa Real lilifungwa na Ruben De Le Red katika Dakika ya 84 alipomhadaa Kipa Van Der Gouw alieingia kuchukua nafasi ya Edwin Van Der Sar
Mchezaji wa siku nyingi wa Man United Jaap Stam akichuana na mchezaji wa Real Madrid
Zinedine Zidane akitaka kumtoka Denis Irwin
Ruud van Nistelrooy akipongezwa na wachezaji wa United baada ya kuwapatia bao
Real Madrid wakimpongeza mchezaji wa zamani wa Liverpool Fernando Morientes
Dwight Yorke akiachia shuti kali mbele ya Francisco Pavon
Claude Makelele kwenye patashika na Paul Scholes akiwa chini hapa, hakika ilikuwa ni fulu burudani
Mechi ilikutanisha wakongwe wazamani katika vilabu vyote kati ya Real Madrid na United
Kipa wa Zamani wa United Edwin van der Sar akishangaa baada ya kufungwa bao
Andy Cole na yeye alikuwa mstari wa mbele kwenye mechi ya Maveteran leo hii.
VIKOSI:
Manchester
United: Van der Sar, van der Gouw; Berg, Blackmore, Irwin,
Johnsen, Martin, Stam; Fortune, Robson, Scholes, Sharpe; Cole, van Nistelrooy,
Yorke.
Real Madrid: Contreras, Sanchez; Cannavaro, Helguera, Hierro, Pavon, Salgado, Sanz; Amavisca, De la Red, Figo, McManaman, Makelele, Zidane; Alfonso, Butragueno, Morientes, van Nistelrooy.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !