Soka la kimataifa kwa mshambuliaji wa Ujerumani, Lukas Podolski liko mashakani iwapo hatatimka Arsenal mwezi Januari.
Podolski
amekuwa nje ya mipango ya kocha Arsene Wenger, jambo linalomfanya
aonekane kwa nadra sana kwenye kikosi cha Arsenal msimu huu.
Bosi
wa Ujerumani Joachim Low amemuonya Podolski kuwa nafasi yake ya
kuitumikia Ujerumani itakuwa hatarini kama hatakuwa na nafasi ya kudumu
kwenye kikosi cha Arsenal.
Lukas
Podolski ameichezea Arsenal mechi nne tu msimu huu, tena zote akitokea
benchi na tayari mchezaji huyo ameweka wazi kuwa yupo tayari kwenda
kusaka changamoto mpya sehemu nyingine ili kuokoa soka yake.
Onyo la Joachim Low linategemewa kumfanya Podolski aongeze spidi ya kutimiza azma yake ya kuondoka Arsenal.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !