Licha ya utata na machafuko yaliyozuka kutokana na mpango wa serikali ya
Tanzania kujenga bomba la gesi kutoka Mtwara Dar es Salaam, bunge la
nchi hiyo limepitisha bajeti ya wizara ya madini na nishati.
Shirika la habari la Reuters limeripoti kwamba kwa kupitisha bajeti hiyo, bunge la Tanzania limeamua kuwa mradi huo unaofadhiliwa na China kwa gharama ya dola bilioni 1.2 uendelee kama ulivyopangwa, licha ya maandamano dhidi yake, ambayo yamesababisha watu wawili kupoteza maisha na mali kadhaa kuharibiwa.
Bunge hilo lilikuwa liipitishe bajeti hiyo ya mwaka 2013/2014 siku ya Jumatano, lakini ghasia zilizozuka juu ya mradi huo wa bomba la gesi zililazimisha bunge kusitisha shughuli zake kwa muda. Hatimaye, siku ya Jumamosi (tarehe 25 Mei), wabunge waliipitisha bajeti na kusema kwamba kazi ya ujenzi wa bomba hilo ingeliendelea hadi kukamilika kwake mwezi Disemba 2014.
HUKU WAKISEMA KWAMBA
"Yeyote anayepinga bomba hili si mwenzetu," Waziri wa Nishati a Madini, Sospeter Muhongo, alitangaza bungeni.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !