Headlines News :
Home » » KOREA KASKAZINI YAONYESHA KIBULI KWA WAPINZANI WAKE KWA KUFYATUA MAKOMBOLAYAKE KATILKA NCHI YA JAPAN

KOREA KASKAZINI YAONYESHA KIBULI KWA WAPINZANI WAKE KWA KUFYATUA MAKOMBOLAYAKE KATILKA NCHI YA JAPAN

Written By kunta kinte on Saturday, May 18, 2013 | 3:05 PM

 
Korea Kaskazini leo imefyatua makombora matatu ya masafa mafupi ndani ya Bahari ya Japan, kama sehemu ya mazoezi ya kijeshi. Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Korea Kusini amesema makombora mawili yalifyatuliwa mapema leo na jingine moja likafyatuliwa saa za mchana. Amesema Korea Kusini inaendelea kuwa katika hali ya tahadhari ili kupambana na hali yoyote ya kitisho inayoweza kusababishwa na serikali ya Korea Kaskazini. Majaribio hayo yanafuatia mazoezi ya pamoja yaliyofanywa na jeshi la wanamaji la Marekani na Korea Kusini mapema wiki hii, na kushutumiwa na Korea Kaskazini kuwa ni uchokozi na matayarisho ya vita.

Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Popular Posts

Comments

blogs zinazotamba

Translate

Popular Post

Flag Counter
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. NDOANO YA HABARI - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template