Jopo lililoundwa na rais kutafuta uwezekano wa kupata makubaliano ya msamaha kwa kundi la Boko Haram, limekutana jana na kiasi ya watuhumiwa 40 kutoka kundi hilo ambao wanashikiliwa jela nje ya mji mkuu Abuja.
Mwenyekiti wa jopo hilo Kabiru Tanimu Turaki amewaambia waandishi habari kuwa wamekuwa na majadiliano mazuri na baadhi ya wafungwa ambao wanashikiliwa kwa madai ya kuwa wanachama wa kundi la Jamaa Ahl al-Sunnah li-da'wa wa al-Jihad, maarufu kama Boko Haram kwa madai ya ugaidi ama vitendo vinavyohusika na matukio kama hivyo.
Hata hivyo hakueleza zaidi kuhusu yale yaliyojadiliwa na jopo hilo.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !